Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:42

Uganda yasema Ongwen atakabidhiwa ICC


Wanajeshi wa Uganda People's Defence Force wakifanya doria msituni huko CAR kulisaka kundi la LRA
Wanajeshi wa Uganda People's Defence Force wakifanya doria msituni huko CAR kulisaka kundi la LRA

Uganda inasema kamanda wa juu wa kundi la Lord’s Resistance Army aliyekamatwa wiki iliyopita atakabidhiwa kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Paddy Ankunda alisema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter hapo jumanne kwamba Dominic Ongwen atashtakiwa kwenye mahakama ya ICC huko The Hague.

Jengo la mahakama ya ICC atakapokabidhiwa Ongwen
Jengo la mahakama ya ICC atakapokabidhiwa Ongwen

Alisema Ongwen atakabidhiwa The Hague na maafisa wa Jamhuri ya afrika kati-CAR, ambako Ongwen alijisalimisha mwenyewe hapo Januari sita.

Msemaji wa jeshi la Marekani alisema jumanne kwamba Ongwen yuko chini ya ulinzi wa washauri wa Marekani wanaolisaidia jeshi la kieneo kupambana na jeshi la LRA huko afrika ya kati.

Msemaji huyo alisema inaaminika mwanamme huyo ni Ongwen na awali alijisalimisha kwa kundi la tatu ambalo lilidai kuwa ni sehemu ya kundi la waasi la Seleka.

Alisema aliona taarifa ya Uganda lakini alisema ni mapema mno kuelezea hatua ifuatayo kuhusiana na Ongwen.

Kundi la LRA linashutumiwa kwa mauaji na utekaji nyara maelfu ya watu katika muda wa miongo mitatu iliyopita, kwanza katika upinzani dhidi ya serikali ya Uganda na baadae kuwa na wapiganaji wanaohama hama nchini Congo, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya kati-C.A.R.

Dominic Ongwen
Dominic Ongwen

Ongwen ni mmoja wa viongozi watano wa LRA wanaoshtakiwa na ICC kwa uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu .

Kundi moja la haki za binadamu la The Enough Project linasema Ongwen alitekwa nyara na kundi la LRA akiwa mtoto mwaka 1990 na hatimaye alilelewa na kuwa kamanda wa cheo cha juu katika kundi hilo la waasi.

XS
SM
MD
LG