Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:53

Uganda yarejesha masharti ya usafiri kwasababu ya virusi vya corona


Mtu na mkewe wakisubiri kupata chanjo ya COVID-19 katika kituo cha afya cha Butanda magharibi mwa Uganda, April 27, 2021.
Mtu na mkewe wakisubiri kupata chanjo ya COVID-19 katika kituo cha afya cha Butanda magharibi mwa Uganda, April 27, 2021.

Waganda wanaoishi maeneo ya mashambani wanalazimika kutembea kwa saa nyingi  kufika mjini

Uganda imerejesha tena masharti ya usafiri kwasababu ya virusi vya corona mpaka mwisho wa mwezi Julai hatua ambayo itabana uwezo wa watu wengi kujikimu kimaisha. Wachuuzi wa mitaani wamelazimika kutumia baiskeli, kutembea mwendo mrefu au kulala sokoni.

Huku maambukizi ya virusi vya corona yakiwa yamepanda na hospitali zikiwa zimeelemewa, Uganda imerejesha tena masharti ya kufunga shughuli mpaka July.

Usafiri umepigwa marufuku, wafanyakazi muhimu wameruhusiwa kuingia mjini.

Wakati ni lengo ni kuokoa maisha, kwa mara nyingine tena kujikimu kimaisha itakuwa ni mapambano kwa wafanyabiashara kama Saudha Namaga, mmoja wa wengi waliolazimika kulala sokoni anamuomba Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kulegeza masharti.

Hali ni mbaya sana kwa maduka ambayo hayauzi vyakula, mamlaka ya Uganda imeamuru yafungwe.

Polisi wa Uganda wamepelekwa kuimarisha amri hizo. Mwenyekiti wa eneo Bashir Muwonge anasema bila ya msaada maduka mengi hayatadumu.

Waganda wanaoishi maeneo ya mashambani wanalazimika kutembea kwa saa nyingi kufika mjini.

Lydia Nambogo alitembea kwa zaidi ya kilometa tano kwenda mjini kuchukua akiba yake ya hela ili aweze kuihudumia familia yake, lakini alipofika alikuta benki imefungwa anasema "nimekuwa nikiuza chakula, na nilikuwa najipatia pesa kidogo ili kuhududmia familia yangu. Lakini tumefngiwa na hatujui kitakachofuata. Serikali haitupi chakula. Basa watupe walau akiba yetu kidogo.”

Mara ya kwanza Uganda kufunga shughuli ilikuwa March mwaka jana, serikali ilitoa unga na maharage kwa watu maskini wanaoishi mjini, ambapo wengi wana matumaini kuwa hiyo itarejewa tena hivi sasa.

Tutatumia njia rahisi, baadhi ya mipango rahisi ya kuwapatia msaada. Na watu walio katika mazingira hatarishi wanajulikana.

Wakati huo huo, waganda wanaweza kusubiri wimbi la karibuni la Covid 19 lipungue wakati wakijitahidi kujikimu kimaisha.

XS
SM
MD
LG