Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 00:09

Uganda yafikiria kuondoa wanajeshi wake Somalia


Sehemu ya jeshi la Uganda likijiandaa kwenda nchini Somalia.
Sehemu ya jeshi la Uganda likijiandaa kwenda nchini Somalia.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema nchi yake itafikiria upya mipango ya kuondoa wanajeshi wake Somalia kama operesheni thabiti za Umoja wa Afrika-AU huko zitakwenda katika mwelekeo sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wa usalama wa kieneo mjini Kampala Jumatatu, Museveni alisema operesheni za kijeshi nchini Somalia hazijafanya kazi kwa mafanikio. Museveni alisema sababu yetu kuu ya kwenda Somalia ilikuwa ni kuwasaidia watu wa Somalia kuunda jeshi lao wenyewe, lakini baada ya miaka tisa hatujaweza kuunda jeshi.

Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Aliongeza kwamba hatuwezi kusaidia msaada wa aina hiyo, aina ya mipango mibaya ni kitu ambacho hatuwezi kusaidia. Pia alisema kwamba hatuwezi kuondoa majeshi kama tunaelekea katika mwelekeo sahihi, kuwasaidia watu wa Somalia kujenga taasisi zao wanazozihitaji.

Uganda ilisema mwezi uliopita kwamba ina mpango wa kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Somalia ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao. Uganda ilipeleka wanajeshi wake nchini Somalia mwaka 2007 na ndio mchangiaji mwenye idadi kubwa ya wanajeshi, akichangia zaidi ya wanajeshi 6,000 kati ya wanajeshi 22,000 wa AMISOM.

XS
SM
MD
LG