Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:21

Uganda yaelezea msimamo kuhusiana na vita vya Sudan Kusini


Wapatanishi kwenye mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini wakiwa Addis Ababa, Ethiopia, Januari 13, 2014.
Wapatanishi kwenye mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini wakiwa Addis Ababa, Ethiopia, Januari 13, 2014.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini Uganda anasema nchi inajukumu muhimu katika juhudi za kieneo za kutatua hali ya usalama nchini sudan Kusini licha ya ukosoaji kwamba serikali ya Kampala inadumaza mashauriano ya amani yanayoendelea nchini Ethiopia kati ya pande hasimu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:06 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Fred Opolot anasema makundi ya upinzani nchini Uganda yana mtazamo finyu wa kisiasa katika ukosoaji wao wa jukumu la jeshi la uganda -UPDF, inalolifanya katika kuisaidia serikali ya Rais Salva Kiir huko Juba. Opolot alisema UPDF imekuwepo Sudan Kusini kwa miaka kadhaa hata kabla ya mgogoro huu sasa. Opot anasema, Riek Machar anajua hilo na waganda wanajua, hivyo basi maoni yao hayasaidii.

Riek Machar
Riek Machar
Makamu Rais wa zamani wa Sudan Kusini Riek Machar alishutumu UPDF kwa kusaidia wanajeshi wanaomtii Rais Salva Kiir katika mgogoro huu. Lakini Opolot anakanusha kwamba msaada wa Kampala kwa bwana Kiir unavuruga mashauriano ya amani.

“Jukumu la Uganda sio kudumaza mashauriano ya amani. Kwa hakika jukumu la Uganda nchini Sudan Kusini ni kuhakikisha wanaozozana wanawasiliana, alisema Opolot. Iwapo kama Uganda inavunja sheria yeyote ya kimataifa , kwanza na zaidi ya hapo IGAD, nina uhakika ingeifahamisha Uganda kuhusu hilo. Lakini Uganda inaonekana mwezeshaji wa utaratibu wa hivi sasa katika mapigano yanayoendelea sudan Kusini”.

Makundi ya upinzani nchini Uganda yanasema jukumu la UPDF katika kuisaidia serikali huko Juba litasababisha raia kujikuta kwenye mashambulizi ya ulipizaji kisasi nchini Sudan Kusini. Lakini Opolot hakubaliani na hilo.

Aliwasihi washirika wa bwana Machar kuelezea wasiwasi wao kuhusu kuwepo kwa Uganda nchini Sudan Kusini kwa wapatanishi kwenye mashauriano ya amani yanayoendelea Addis ababa, Ethiopia.
XS
SM
MD
LG