Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 02, 2024 Local time: 07:59

Uganda yawashambulia waasi wa ADF


Jeshi la Uganda latumia makombora kushambulia waasi wa kikundi cha ADF
Jeshi la Uganda latumia makombora kushambulia waasi wa kikundi cha ADF

Jeshi la Uganda (UPDF) limesema kuwa limeshambulia kambi kadhaa za waasi wa kikundi cha ADF katika upande wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa tamko jeshi la UPDF, vikosi vyake vilifanya mashambulizi ili kuzuia waasi hao kufanya mashambulizi waliokuwa wameyapanga baada ya kupata taarifa za kijasusi juu ya mpango huo.

Katika hatua hiyo ya kuzuia shambulizi hilo, Ijumaa mchana jeshi la UPDF ilishambulia kambi za waasi katika eneo la mashariki mwa DRC. Magaidi wa ADF wanaweza kuvuta muda lakini watafikiwa pahali popote wanapojificha!” tamko hilo lililotolewa na msemaji wa jeshi Brigedia Richard Karemire limeeleza.

Karemire ameiambia Xinhua katika mahojiano baadae kwamba jeshi lilitumia ndege za kivita kushambulia.

“Majeshi yetu hayajaingia DRC. Tulitumia ndege za kivita na makombora ya masafa marefu kufanya mashambulizi hayo,” amesema.

Mashambulizi haya ya kushtukiza yamefanyika wiki mbili baada ya kikundi cha waasi Disemba 7 kushambulia walinda amani wa UN huko upande wa mashariki wa DRC, jimbo la Kivu Kaskazini, na kuua askari wa Tanzania walinda amani 14, askari wa DRC 5 na kujeruhi wengine 44.

XS
SM
MD
LG