Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 16, 2025 Local time: 06:32

Uganda yabakia kwenye kiwango cha kipato cha chini, Benki ya Dunia yasema


Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Benki ya Dunia, imesema kwamba Uganda inasalia kuwa nchi ya kipato cha chini, wiki mbili baada ya Rais Yoweri Museveni na waziri wa fedha Matia Kasaija kusema uchumi wa nchi hiyo umepanda hadi kufikia kiwango cha kipato cha kati.

Pato la taifa lilikua kwa asilimia 4.3 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kutokana na kufufuliwa kwa sekta ya huduma, baada ya kuondolewa kwa masharti ya usafiri na mikusanyiko ya kijamii, na kuimarishwa kwa sekta ya habari na mawasiliano.

Lakini, kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia, hayakutosha kuiinua nchi hiyo kufikia kiwango cha kipato cha kati. Benki ya Dunia ilisema mapato ya Uganda kwa kila mtu yaliimarika sana kati ya 2001 na 2011, na kupunguza pengo kutoka asilimia 75 mwaka 1994 hadi asilimia 17 mwishoni mwa kipindi hicho.

Tangu wakati huo, hata hivyo, pengo limesalia kati ya asilimia 19 hadi 26, kwani kiwango cha juu cha idadi ya watu kilichangia katika kupungua kwa ukuaji wa uchumi. Ripoti hiyo, ambayo ni tathmini ya kila mwaka ya uchumi, ilisema pato la taifa la Uganda (GNI) kwa kila mtu lilifikia takriban dola 840 mwaka wa 2021 na limeongezeka kidogo tu katika mwaka huo, na kuiacha nchi hiyo chini ya mapato ya chini.

XS
SM
MD
LG