Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 02:39

Uganda: Watu 3 wauawa katika mapambano na polisi


Maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na ghasia wanambeba mmoja wa wafuasi wa mgombea urais Bobi Wine, katika wilaya ya Luuka, Mashariki mwa nchi hiyo. Nov 18, 2020.
Maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na ghasia wanambeba mmoja wa wafuasi wa mgombea urais Bobi Wine, katika wilaya ya Luuka, Mashariki mwa nchi hiyo. Nov 18, 2020.

Watu 3 wameuwawa jumatano mjini Kampala katika mpambano kati ya polisi na wafuasi wa mgombea urais Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine, polisi wamesema.

Mauaji hayo yametokea wakati wafuasi wa Bobi Wine wakiandamana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao.

Mapema asubuhi, Wine alikamatwa na polisi kabla ya kuelekea kwenye kampeni yake katika wilaya ya Luuka iliyo mashariki mwa Uganda, hali ambayo ilipelekea wafuasi wake kuandamana katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Baadaye polisi walimfungulia mashtaka Bobi Wine kwa "kufanya kitendo ambacho kinaweza kusababisha kusambaa kwa virusi vya covid 19," muandishi wa sauti ya Amerika mjini Kampala amearifu.

Polisi walimshtumu kwamba amekiuka masharti ya tume ya taifa ya uchaguzi, kwa kuhamasisha zaidi ya wafwasi wake 200 kuhudhuria kampeni yake, wakati tume hiyo inaruhusu watu wasiozidi 100 kushiriki kwenye kampeni za wagombea urais, ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Waliongeza kuwa mwanasiasa huyo amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Nalufenya, katika mji wa Jinja, mashariki mwa mji mkuu Kampala.

Wakati huo huo mgombea mwingine wa urais kwa tikiti ya chama cha upinzani FDC, Patrick Oboi Amriat, amechiliwa huru baada ya kukamatwa na polisi wa mjini Gulu kwa tuhuma za kukiuka kanuni za kujikinga na maambukizi ya Corona.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Kampala, ameripoti kuwa baada ya taarifa ya kukamatwa kwa Bobi Wine, wafuasi wake pia wameandamana katika mji wa Masaka, kati kati mwa Uganda, na kuweka vizuizi barabarani.

Polisi walithibitisha kwamba watu 34 wamejeruhiwa katika mfarakano huo.

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani wameripotiwa kusitisha kampeni zao kama ishara ya kuungana na wafuasi wa Bobi Wine kupinga hatua zinazochukuliwa na polisi dhidi yao.

Tangu kampeni za uchaguzi wa rais wa mwaka wa 2021 kuanza, Bobi Wine amekuwa akizozana na polisi ambao wamemkamata mara kwa mara, wakimshtumu kukiuka maagizo ya serikali na tume ya uchaguzi ya kupambana na janga la Corona, madai ambayo anakusha.

-Imetayarishwa na Patrickl Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG