Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 22:52

Maandamano ya kwenda kazini kwa mikuu yaanza tena Uganda


Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza besigye, akiwahutubia wafuasi wake katika mkutano unaopinga kuongezeka kwa gharama za maisha huko Namungoona, Kampala

Maandamano ya kwenda Kazini kwa Miguu yameanza tena Uganda kwa kupewa jina la "Walk to Work Reload".

Viongozi wa upinzani nchini Uganda wamezindua upya malalamiko yao ya kisiasa yaliyofanyika mwaka jana ya Kwenda Kazini kwa Miguu, ikiwa ni mfululizo wa maandamano yaliyosababisha kukamatwa watu pamoja na mapambano na polisi.

Maandamano haya mapya yamepwa jina la “Walk to Work Reload” ikiwa ni vuguvugu la malalamiko dhidi ya serikali ya Rais Yoweri Museveni, na yanaendelea kuanzia mahala walipoishia mwaka jana wakati walipoanza kupata umashuhuri wa kitaifa na kimataifa. Wameamua kufanya mkutano wa hadhara kila siku kwa muda wa wiki moja.

Kwa mara nyingine, Kizza Besigye, kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change-FDC, amekua na mikutano ya hadhara kuzungumzia dhidi ya rushwa, utawala mbaya na kuongezeka kwa gharama za maisha. Na kwa mara nyingine Besigye na wafuasi wake wamebughudhiwa, wamefyatuliwa gesi ya kutoa machozi na kukamatwa siku ya Jumatano.

Wiki iliyopita, Besigye na idadi kadhaa ya wanasiasa na waandaaji wa mikutano hiyo walikamatwa kwa muda kabla ya kufanyika mkutano.

Msemaji wa polisi Judith Nabakooba aliwaambia waandishi wa habari kwamba walikuwa na haki zote za kuwakamata viongozi wa Walk to Work. “Walikamatwa ili kuwazuia wasiweze kushiriki katika vitendo ambavyo vingepelekea kuharibu mali, kujijeruhi wenyewe na wengine, na pia kuzuia barabara kuu. Kisheria tunatakiwa kuchukua hatua kama hizo kama tunaona kwamba kuna uwezekano wa kuvurugika amani.”

Mary Okurut, waziri wa habari na muelekeo wa kitaifa nchini Uganda, aliwaambia waandishi wa habari kwamba hatua ya polisi ilikuwa ni kuzuia kile alichokiita “uasi wa wananchi na mtafaruku.” Maandamano kadhaa yamefanywa mjini Kampala na kila wakati polisi wamekuwa wakiwafyatulia waandamanaji gesi ya kutoa machozi. Besigye anadai kwamba utumiaji huu wa nguvu kupita kiasi ni utumiaji mbaya wa madaraka.

XS
SM
MD
LG