Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 04:27

Unyanyasaji wa ngono ni tatizo kubwa katika mataifa ya maziwa makuu


Unyanyasaji wa ngono na jinsia bado ni tatizo katika eneo la maziwa makuu

Shirika la Refugee Law Project, lazindua kampeni ya kupambana na unyanyasaji wa jinsia na ngono unaofanyiwa wakimbizi

Unyanyasaji wa ngono na jinsia ni suala ambalo limekuwa likizungumziwa kwa muda mrefu kote ulimwenguni, lakini imeelezwa wiki hii unyanyasaji wa kingono hasa kwenye eneo la maziwa makuu bado ni tatizo kubwa.

Shirika lisilo la kiserikali la Refugee Law Project, ambalo hutetea haki za wakimbizi na wakimbizi walio ndani ya nchi yao limeanzisha kampeni ya wiki moja iliyopewa mada ya "Muungano wa wakimbizi na jamii kupinga unyanyasaji wa kingono."

Madhumuni ya kampeni hii ni kuuhamasisha ulimwengu kuhusu masuala ambayo yanaandamana na jinsia na ngono.

Suala la ubakaji wa wakimbizi pia litapewa kipaumbele. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wakimbizi-UNHCR, linasema wakimbizi wengi nchini Uganda wanatoka katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.

Ubakaji mara kwa mara utumika kama silaha . Shirika la Refugee Law Project linasema kesi za wakimbizi kubakwa zimeongezeka pamoja na kesi za wanawake kuahidiwa kupatiwa kazi nchi nyingine , lakini wakishaondoka nchini mwao wanatumiwa kama watumwa wa ngono. Madai yao hayakuungwa mkono na takwimu zozote.

Dr.Chris Dolan ni mkurugenzi wa shirika hili, anasema “hatuwezi kusema ni watu wangapi wananyanyaswa lakini tunaweza kuanza kuhesabu watu tunaowahudumia na ambao wamewapoteza jamaa zao”.

Dr.Dolan alisema itakuwa vigumu kwao kuzungumzia suala la jinsia na haki za binadamu bila kuwazungumzia watu wanaoshiriki kwenye mapenzi ya jinsia moja ambao pia wamekuwa wakinyanyaswa ki-jinsia.

Wakati huo huo naibu waziri wa maswala ya jinsia nchini Uganda, Suleiman Madada akijibu swali la mikakati ambayo imewekwa na serikali ili kuwalinda wakimbizi wasinyanyaswe alisema “siwezi kuthibitisha kuwa tuna moja lakini tunavyo vipengele hapa na pale ambavyo tunaweza kuviangalia lakini itabidi niviangalie vipengele hivi kwa sababu siwezi kuwa mtaalam wa kila kitu hapa”.

XS
SM
MD
LG