Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 11:53

Uganda yawafukuza wakimbizi wa Rwanda


Uganda imewafukuza nchini humo wakimbizi wa Rwanda 1,700 ambao walikuwa wakiomba hifadhi nchini humo. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR- lililaani hatua hiyo ikisema inakiuka misingi ya kimataifa ya kuwahudumia vizuri wakimbizi.

Uganda imewafukuza nchini humo wakimbizi wa Rwanda 1,700 ambao walikuwa wakiomba hifadhi nchini humo. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR- lililaani hatua hiyo ikisema inakiuka misingi ya kimataifa ya kuwahudumia vizuri wakimbizi.

Msemaji mmoja wa shirika hilo, alisema wakimbizi walichukuliwa na polisi baada ya kuwalaghai kwa kuwaahidi hifadhi na chakula. Shirika la habari la Ufaransa - AFP - limemkariri waziri za wakimbizi nchini Uganda, Tarsis Kabwegyere, akisema kila kitu kilifanywa kwa kufuata taratibu. Pia alisema hakukuwa na sababu ya msingi kwa wakimbizi hao kupatiwa hifadhi nchini humo.

Makundi ya wakimbizi huko Kampala yalitoa wito kwa Uganda kuacha haraka kuwaondoa wakimbizi wa Rwanda kutoka kusini-magharibi mwa Uganda. Mkuu wa shirika Refugee Law Project, Chris Dolan, alisema wakimbizi wengi wana khofu ya kuteswa na mahakama za Gacaca zinazotumika nchini Rwanda kushughulikia uhalifu uliofanyika wakati wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Wakimbizi walifukuzwa kutoka makambi ya wakimbizi ya Nakivale na Kyaka huko kusini mwa Uganda. UNHCR ilisema raia 3,200 wa Rwanda wanatafuta hifadhi nchini Uganda tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Shirika hilo lilisema lina wasi wasi maombi ya hifadhi hayakushughulikiwa ipaswavyo baada ya asilimia 98 ya maombi hayo kukataliwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

XS
SM
MD
LG