Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 01:50

Uganda na Sudan zataka kuimarisha uhusiano wao


Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Nchi hizo zimeshutumiana kuunga mkono waasi kutoka pande zote. Khartoum inaishutumu Kampala kuunga mkono waasi katika mkoa wa Darfur.

Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Bakri Hasan Salih na rais wa Uganda Yoweri Museveni ijumaa walifanya majadiliano kuhusu masuala ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili.

Nchi hizo zimeshutumiana kuunga mkono waasi kutoka pande zote. Khartoum inaishutumu Kampala kuunga mkono waasi katika mkoa wa Darfur.

Wakati wa miezi ya hivi karibuni Khartoum ilikubali kwamba waasi wa Sudan hawapo tena Uganda na iliahidi kushirikliana na kampala na kutoa mwito kwa umoja wa Afrika kufanya uchunguzi wa kuwepo waasi wa LRA nchini Sudan.

Katika taarifa kutoka Johanesburg ambapo mkutano unaojadili masuala ya ushirikiano wa Africa na China unafanyika , waziri wa masuala ya kigeni wa Sudan Ibrahim Ghandur alieleza kwamba Sahil na Museven walikutana nje ya mkutano huo mbele ya mawaziri wengine kutoka nchi hizo mbili.

Mkutano huo ulijadili kuhusu ziara ya rais Museven mwezi Septemba uliopita na kutathmini utekelezaji wa matokeo yake. Pia Gandur amesema nchi hizo zilijadili kuhusu ushirikiano wa kamati iliyokubaliwa na nchi hizo mbili wakati wa ziara ya makamu wa rais alipotembelea Uganda mwezi februari mwaka huu.

Ameongeza kuwa mkutano wa tatu utafanyika mjini kampala lakini hakueleza ni wakati gani.

Wakati wa ziara ya Khartoum rais wa Uganda na Sudan walikubaliana kufanya kazi pamoja kurejesha uthabiti Sudan Kusini na katika eneo kwa ujumla na kumaliza mvutano baina ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya makundi ya waasi.

XS
SM
MD
LG