Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:36

Serikali ya Uganda yatakiwa kulipa madeni


Uwekaji wa vifaa kwa ajili ya umeme wa jua umeongezeka huko Soroti, Uganda.
Uwekaji wa vifaa kwa ajili ya umeme wa jua umeongezeka huko Soroti, Uganda.

ripoti ya mkaguzi mkuu inaitaka serikali kuacha kulipa wafanyakazi hewa na kusitisha kulipa watumishi wa serikali maradufu kila mwezi.

Ripoti hiyo ya 2015/16 imeikosoa serikali kutokana na kukosa kulipa madeni yake na kuendelea kukopa kutoka benki za ndani ya nchi, ikieleza kitendo hicho ni hatari kwa uchumi wa taifa.

Mwandishi wa VOA, Kennes Bwire amesema ripoti hiyo inaashiria hali ngumu ya kiuchumi ikionyesha jinsi gani serikali imejiongezea mzigo wa deni la shilingi trilioni 6.5 katika kipindi cha miaka mitatu, kuanzia mwaka 2013.

“Serikali inaendelea kukopa kutoka benki zilizopo ndani ya nchi, wakati tayari inadaiwa kiasi cha shilingi trilioni 2.7, jambo linalopelekea benki nchini kuongeza viwango vya riba na kuathiri biashara ndani ya nchi,” alisema mkaguzi mkuu wa serikali, John Muwanga.

Ripoti hiyo imeendelea kuitaka serikali kuacha mara moja kulipa mishahara wafanyakazi hewa huku baadhi ya watumishi wa umma wakipokea mishahara mara dufu kila mwezi na malipo ya pensheni yasiyokuwa na nyaraka kuthibitisha nani anayepokea malipo hayo.

Mkaguzi mkuu amesema: “Serikali inaendelea kupata hasara kubwa ya asilimia 90 kutokana na kushindwa katika kesi dhidi yake mahakamani.”

“Kinachotutia wasiwasi ni kwamba hasara hii imekuwa ikiongezeka kwa kasi sana katika kipindi cha miaka mitatu kutoka shilingi trilioni 2.3 hadi trilioni 6.5’,” amesema.

Aliongeza kuwa sasa kinachotakiwa ni kamati za bunge zinazohusika na uadilifu kuwachunguza viongozi serikalini katika ofisi husika ili kupekua zaidi masuala yaliyotajwa katika ripoti hiyo.

Ripoti imeendelea kuelezea kuwa serikali imezembea katika kulipa madeni yake huku ikidaiwa kiasi cha shilingi trilioni 18.1 kama mikopo.

XS
SM
MD
LG