Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:12

Uganda kutuma wanajeshi 1000 DRC


Wanajeshi wa Uganda wakiwa Beni, DRC Dec 8,2021
Wanajeshi wa Uganda wakiwa Beni, DRC Dec 8,2021

Serikali ya Uganda imesema itatuma wanajeshi wake 1000 katika nchi jirani ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kufikia mwishoni mwa mwezi huu.

Wanajeshi hao wanaingia mashariki mwa DRC chini ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika mashariki.

Nchi saba za jumuiya ya Afrika mashariki zilikubaliana kutuma wanajeshi kupambana na makundi ya waasi ambayo yamesababisha ukosefu wa usalama mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa miongo kadhaa.

Uganda itakuwa nchi ya tatu kutuma wanajeshi wake nchini Congo baada ya Kenya na Burundi.

Msemaji wa jeshi la Uganda Brigendia Jenerali Felix Kulaigye amesema kwamba wanajeshi wa Uganda wapo tayari kusaidia katika kurejesha amani katika nchi hiyo Jirani.

Hata hivyo, baadhi ya makundi ya kijamii yamekuwa yakidai kwamba Uganda inahusika pakubwa na vita vianvyoendelea Congo, yakidai kwamba inaunga mkono waasi wa M23.

Tayari Uganda ina wanajeshi wake nchini DRC, wanaopigana na kundi la waasi la Allied democratic Forces ADF.

Uganda imelipa DRC dola milioni 65 kama sehemu yad ola milioni 325 ilizoagizwa kulipa Congo kwa hasara ambayo Congo ilipata wakati wanajeshi wa Uganda waliingia nchini humo miaka ya 1990.

Licha ya mabilioni ya dola kutumika kwa kikosi cha jeshi la umoja wa mataifa kulinda amani nchini DRC, bado kuna zaidi ya makundi ya waasi 120 likiwemo kundi la M23, yanayopigana na wanajeshi wa serikali.

DRC imeshutumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23, amadai ambayo Rwanda imekuwa ikikana kila mara.

XS
SM
MD
LG