Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 13:14

Besigye aachiliwa huru na polisi


Kizza Besigye aachiliwa huru baada ya kukamatwa na polisi mjini Kampala, Uganda.
Kizza Besigye aachiliwa huru baada ya kukamatwa na polisi mjini Kampala, Uganda.

Na Sunday Shomari, Kampala

Mgombea urais wa chama cha upinzani cha FDC nchini Uganda, Kizza Besigye, ameachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka Jumatatu alasiri baada ya kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Kira Road nchi mjini kampala kwa masaa kadhaa.

Mapema Jumatatu polisi walilipua mabomu ya gesi ya machozi na kuwatawanya wafuasi wa Besigye ambao walikuwa wanaandamana kwenye barabara za mji wa huo kabla ya kumtia mbaroni pamoja na watu wengine kadhaa.

Mahojiano na Sunday Shomari
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:55 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Gari la mwanasiasa huyo lilikuwa likipitia barabara ya Jinja na polisi wanasema alikamatwa kwa sababu ya kutatiza uchukuzi mjini.

Akizungumza na Sauti ya Amerika muda mfupi kabla ya kuchukuliwa na polisi, Bw Besigye alisema anasikitishwa "na hatua ya serikali ya kuukandamiza upiinzani."

Mkuu wa Polisi Jenerali Uganda Kalekezi Kayihura amethibitisha kwamba polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani lakini akakanusha habari kwamba Bw Besigye amekamatwa.

Lakini polisi walisema kwamba Besigye alikiuka sheria na kukaidi agizo la polisi la kutoingia katikati mwa mji huo

Wafuasi wa Besigye, Kampala
Wafuasi wa Besigye, Kampala

“Besigye yuko huru kufanya kampeni mjini Kampala lakini sharti atii maagizo ya Tume ya Uchaguzi na Polisi ambayo yanaharamisha siasa katikati mwa jiji,” msemaji wa polisi Fred Enanga ameambia wanahabari mjini Kampala

Msemaji wa FDC anasema Dr.Besigye amenyang'anywa walinzi aliokuwa amepewa na watu aliokuwa nao wamepigwa viboko pamoja na mabomu ya machozi.

Katika shambulizi la Jumatatu asubuhi mtu mmoja alijeruhiwa vibaya mkononi na risasi ya bandia na watoto kadhaa walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa kutokana na kukanyagana na kusukumana kulikotokea.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake baada ya ghasia hizo Besigye aliwaasa wafuasi wake kutoogopa akisema hizi ni njama za Polisi kuwatisha wafuasi wake amewataka wajitokeze kwa wingi siku ya Alhamisi Februari 18 ili wapigie kura mabadiliko.

Wagombea wengine Amama Mbabazi alikuwa akipiga kampeni katika eneo la Kaskazini mashariki la Kaberamaido na rais Yoweri Museveni alikuwa katika maeneo ya Soroti,Mbale na Tororo.

Jumanne ndio siku ya mwisho ya kampeni za wagombea urais nchini Uganda.

XS
SM
MD
LG