Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 13:29

Burundi:Kosa la Uhaini kwa mwandishi wa habari


Moja ya mitandao ya habari duniani.
Moja ya mitandao ya habari duniani.

Kundi moja la kimataifa la kutetea haki za vyombo vya habari, limeeleza kusikitishwa kwake juu ya kukamatwa kwa mwandishi wa habari mmoja nchini Burundi, ambaye aliandika makala inayokosoa jeshi la nchi hiyo.

Kundi moja la kimataifa la kutetea haki za vyombo vya habari, limeeleza kusikitishwa kwake juu ya kukamatwa kwa mwandishi wa habari mmoja nchini Burundi, ambaye aliandika makala inayokosoa jeshi la nchi hiyo.

Kundi hilo la Committee to Protect Journalists-CPJ, lenye makao yake New York, linasema Jean-Claude Kavumbagu, mhariri wa gazeti binafsi la Net Press, ameshtakiwa kwa kosa la uhaini. Kavumbagu alikamatwa Jumamosi, baada ya gazeti la Net Press kuchapisha habari zinazohoji uwezo wa majeshi ya Burundi kuzuia shambulizi la kigaidi katika ardhi ya Burundi, kama shambulizi la mabomu lililofanywa hivi karibuni katika nchi jirani ya Uganda. CPJ inasema shtaka la uhaini ni kubwa sana.

Wanasema Kavumbagu anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha jela, ikiwa atakutwa na hatia. Burundi na Uganda zimechangia vikosi vya wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa Afrika wanaohudumu nchini Somalia.

Kundi la wanamgambo la al-Shabab kutoka Somalia, lilidai kufanya mashambulizi mawili ya mabomu wiki iliyopita nchini Uganda, likisema mashambulizi hayo yalifanywa kulipiza kisasi vifo vya raia wa Somalia vilivyosababishwa na majeshi ya Umoja wa Afrika huko Mogadishu. Milipuko hiyo iliuwa watu 76 na ililenga hoteli moja na klabu moja ambapo watu walikusanyika kutazama fainali za mwisho za Kombe la Dunia.


XS
SM
MD
LG