Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 04:44

Uganda: Ofisi ya UN ya haki za binadamu yafungwa


Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema Ijumaa kuwa imelazimika kufunga ofisi yake nchini Uganda na kwamba itasitisha rasmi shughuli zake nchini humo Jumamosi.

Katika taarifa yake ya kutangaza kufungwa, Volker Turk, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu alisema, "Ninasikitika kwamba ofisi yetu nchini Uganda ililazimika kufungwa baada ya miaka 18, ambapo tuliweza kufanya kazi kwa karibu na mashirika ya kiraia, na watu wa tabaka mbalimbali nchini Uganda, pamoja na kushirikiana na taasisi za serikali kwa ajili ya kukuza na kulinda haki za binadamu za Waganda wote.”

Msemaji wa kamishna mkuu, Ravina Sham-dasani, aliiambia VOA kwamba serikali iliifahamisha Turk mwezi Februari kwamba haitasaini upya mkataba wa nchi mwenyeji, ambao unaruhusu ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kufanya kazi nchini humo.

"Kwa maoni yao, Uganda ilikuwa na uwezo wake wa kusimamia hali ya haki za binadamu ambapo ofisi ya haki za binadamu haikuhitajika tena," alisema.

"Sisi, bila shaka, tunajutia sana uamuzi huu. Tumekuwa nchini Uganda kwa miaka 18…na tumejaribu kutumika kama daraja kati ya serikali na mashirika ya kiraia.”

Sauti ya Amerika ilijaribu kuwasiliana na ujumbe wa Uganda mjini Geneva, Uswizi, lakini haikupata maoni yoyote kuhusu kwa nini serikali iliamua kuliondoa shirika la Umoja wa Mataifa nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG