Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:05

Uganda: Gazeti la Monitor lakata rufaa kwenye Mahakama ya juu kupinga uamzi wa fidia kwa afisa mkuu wa serikali

Wanaharataki wa kutetea uhuru wa habari za mitandaoni wakishikilia mabango wakati wakiandamana baada ya kuwasilisha shauri kwenye Mahakama ya katiba mjini Kampala dhidi ya sheria mpya inayoadhibu baadhi ya shughuli kwenye mtandao wa intaneti, Oktoba 17, 2022. Picha ya AP

Chombo huru cha habari nchini Uganda Jumapili kimesema kwamba kinakata rufaa kwenye Mahakama ya juu ya nchi hiyo kupinga uamuzi wenye utata wa fidia kwa kumkashifu afisa mkuu wa serikali katika kesi kubwa ya ufisadi.

Majaji wa Mahakama ya rufaa wiki iliyopita waliliamuru gazeti la Monitor kulipa fidia ya dola 120,000 kwa Pius Bigirimana kutokana na msururu wa makala zilizochapishwa kuanzia mwaka 2012 hadi 2015, ukiwa uamuzi mkubwa wa kifedha dhidi ya vyombo vya habari nchini Uganda.

Ripoti zinazohusiana na kashfa ya ufisadi ambapo dola milioni 40 za mradi wa kukarabati eneo la kaskazini mwa Uganda baada ya uasi mbaya wa kundi la Lord Resistance Army (LRA) la Joseph Kony dhidi ya Rais Yoweri Museveni, ziliibwa.

Jaji kiongozi wa mahakama ya rufaa Elisabeth Musoke alisema Alhamisi kwamba Monitor ilimwonyesha Bigirimana, katibu mkuu kwenye ofisi ya waziri mkuu wakati ubadhirifu huo ulipotangazwa hadharani, kama mtumishi wa umma mfisadi, mdanganyifu na asiyewajibishwa.

XS
SM
MD
LG