Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:07

Kampeni za uchaguzi mkuu kuanza Uganda


Uganda President Yoweri Museveni, kushoto; na mpinzani wake kutoka chama cha Forum for Democratic Change’s Dr. Kizza Besigye, kulia.
Uganda President Yoweri Museveni, kushoto; na mpinzani wake kutoka chama cha Forum for Democratic Change’s Dr. Kizza Besigye, kulia.
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:23 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kampeni rasmi za uchaguzi wa rais nchini Uganda zinaanza Jumatatu wakati wagombea ikiwa pamoja na rais aliye madarakani Yoweri Museveni, waziri mkuu wa zamani Patrick Amama Mbabazi , pamoja na mkuu wa upinzani Dr. Kizza Besigye wamekamilisha zoezi la kuimarisha timu zao za kampeni.

Tume hiyo imeonya wagombea wote nane wakati wanapofanya kampeni zao , kutokutumia lugha zenye kuleta mgawanyiko wa kikabila au kidini, ambao unaweza kuleta hali ya mivutano na kupelekea ghasia .

Maafisa wanasema tume hiyo ya uchaguzi imeeleza kuwa inatekeleza hatua za kuhakikisha uchaguzi wa rais utakuwa huru, haki na wazi.

Jotham Taremwa msemaji wa tume ya uchaguzi anasema tume hiyo imetia saini waraka wa makubaliano na vyama vya kisiasa kuwahimiza kufuatwa maelezo ya makubaliano hayo.

Bw Taremwa amesema hilo linahakikisha utaratibu upo sawa kwa wote , katika harakati za kuwania kura za urais.

Hata hivyo makundi ya upinzani yameshutumu idara za usalama nchini humo kwa kumpendelea rais Museveni na chama chake tawala cha National Resistance Movement, NRM. Hata hivyo tume ya uchaguzi imekana hilo.

XS
SM
MD
LG