Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 05:14

Watu 49 watia nia kugombea urais Uganda


Viongozi wa upinzani Uganda, kutoka kushoto Dr. Kizza Besigye, Amama Mbabazi na Norber Mao.
Viongozi wa upinzani Uganda, kutoka kushoto Dr. Kizza Besigye, Amama Mbabazi na Norber Mao.

Watu 49 wameeleza nia yao ya kuwania urais nchini Uganda, wakiwa wamechukua fumu za kuwania nafasi hiyo kutoka kwa tume ya uchaguzi. Idadi hiyo imeongezeka baada ya muungano wa vyama vya upinzani, The Democratic Alliance - TDA, kukosa kumteua mgombea mmoja kati ya aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi na Dk. Kiiza Besigye. Wengi wa wanaotafuta kiti cha urais hawana vyama vya kisiasa na watakampeni kama waaniaji binafsi.

Msemaji wa tume ya uchaguzi Paul Bukenya amesema kwamba idadi kubwa ya wanaowania urais hawana vyama vya kisiasa.

Watu 49 kuwania urais Uganda
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

“Watu 49 walichukua fomu, 10 kutoka vyama vilivyosajiliwa, na 39 kati yao hawana vyama. Tumekuwa tukizipokea fomu zilizojazwa na kufikia sasa, saba pekee zimerudishwa. Tunadurusu fomu hizo, na tutaweza kuwachuja baadhi yao kufikia wiki ijayo” amesema Bukenya.

Idadi kubwa ya wanaotaka kuwania urais nchini Uganda, imezua maoni tofauti kati ya wapiga kura, wengi wakiwa na maoni kwamba hii itampa rais wa sasa Yoweri Museeveni nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi huo.

Monday Amazima ni mchambuzi wa siasa anayehisi kwamba iwapo wanachama wa upinzani hawataimarisha juhudi zao kuwafikia wapiga kura, Museveni atasalia madarakani.

“Idadi kubwa ya wagombezi hasa kiti cha urais, huenda ikampa rais Museveni kurejea madarakani na pia huenda ikamnyima nafasi kwa sababu unajua katiba inasema kwamba mtu kutangazwa kama mshindi anastahili apate asilimia hamsini na zaidi. Kwa hivyo wagombea wakiwa na nguvu, huenda wakamnyima nafasi lakini wakiwa ni wanasiasa wa kubahatisha kama wanavyoonekana, basi watampa nafasi ya kuendelea kuwa madarakani” amesema Amazima.

Tume ya uchaguzi ya Uganda imeeleza kwamba inakaribia kuwapiga msasa wote waliochukua fomu hizo, wiki ijayo.

Bw. Bukenya ameeleza kwamba shughuli hiyo ni rahisi na tayari maafisa wake wanashughulikia fomu zilizorejeshwa kwa haraka.

Ilitarajiwa kwamba wanasiasa wa upinzani wangeungana na kumteua mmoja kati yao kushindana na rais Museveni lakini jaribio la kuunda muungano lilishinidikana. Hii ni baada ya Dkt. Kiiza Besigye wa Forum for Democratic change(FDC) na Amama Mbabazi wa ‘Go Forward’, kukosa kukubaliana ni nani kati yao angemenyana na rais Museveni kwa tiketi ya muungano wa Democratic Alliance – TDA, licha ya muungano huo kupata umaarufu mkubwa.

Katiba ya Uganda inamruhusu raia wake yeyote mwenye umri wa miaka 35 na zaidi, aliye na kisomo cha kidato cha sita kuwania urais.

Uchaguzi mkuu wa Uganda utaandaliwa kati ya Februari 12 na Machi 12 mwaka 2016.

XS
SM
MD
LG