Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 00:00

Uganda: Chanjo ya majaribio dhidi ya Ebola inatengenezwa


Madaktari wakivaa mavazi maalum ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ebola katika chumba maalum cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola, Entebbe, Uganda Okt. 20, 2022

Kampuni ya kutengeneza dawa, Merck& Co (MRK.N), imesema kwamba inapanga kutengeneza chanjo ya majaribio dhidi ya virusi vya ebola na itaitoa bure, kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko wa Ebola aina ya Sudan, ambao umeripotiwa nchini Uganda.

Chanjo hiyo ya majaribio itatolewa kwa shirika lisilokuwa la kiserikali linalofanya utafiti kuhusiana na ugonjwa wa Ebola nchini Uganda.

Uganda imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya mlipuko wa virusi hivyo ambavyo ni tofauti na vile vinavyoiathiri nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mashirika hayo yatapokea chanjo hizo ambazo zimethibitishwa kuwa na uwezo wa kupambana na virusi vya Ebola aina ya Sudan ambavyo mpaka sasa havina chanjo.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya Uganda na Shirika la Afya Duniani WHO, virusi vya Ebola vimesambaa nchini Uganda na kusababisha vifo vya watu takriban 44.

Watu wengine 90 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola.

Aidha, Kampuni ya Merik imeahidi kutoa msaada wa dozi 50,000 kwa shirika la GAVI mwishoni mwa mwaka huu, kwa hivi sasa inafanya mawasiliano na shirika hilo la misaada ya kiafya hususan milipuko ya magonjwa ya kuambukiza yanayoikabili dunia ikiwemo UKIMWI na kifua kikuu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG