Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:07

Bunge la Uganda lakaidi amri ya mahakama


Kikao cha bunge nchini Uganda
Kikao cha bunge nchini Uganda

Spika wa bunge la Uganda amesimamisha majadiliano Jumanne na kusitisha shughuli za kamati zote na kuamuru wabunge

Spika wa bunge la Uganda amesimamisha majadiliano Jumanne na kusitisha shughuli za kamati zote na kuamuru wabunge warudi nyumbani, mpaka mwanasheria wa serikali atapoondoa amri ya mahakama bungeni ambayo ameiita ni 'upuuzi'.

Spika Rebecca Kadaaga amekaidi amri ya muda iliyotolewa na mahakama ya katiba inayokataza mtu yeyote kujadili au kuchunguza ubadhirifu wa shilingi bilioni 6 za Uganda zilizotolewa na rais Yoweri Museveni kuwapongeza maafisa wa serikali.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya VOA, Kennes Bwire ameripoti kuwa naibu jaji mkuu Stephen Kavuma, amezingatia ombi la wakili wa tume ya uchaguzi Erick Sabiti, kwamba bunge au mtu yeyote yule, hana mamlaka ya kuchunguza uamuzi wa rais, kulingana na katiba ya Uganda.

Jaji aonya vyombo vya habari

Jaji Kavuma pia ameamrisha vyombo vya habari kukoma mara moja kuandika, kujadili, au kuchunguza sakata hilo la mabilioni ya pesa.

Hata hivyo spika wa bunge, Rebecca Kadaaga mapema leo aliwaruhusu wabunge kuwasilisha hoja kuhusu maafisa 42 wa serikali waliomuomba rais Museveni kuwazawadiya shilingi bilioni 6 baada ya kushinda kesi iliyokuwa inaikabili kampuni ya mafuta ya Tallow baada ya kukwepa kulipa ushuru.

Spika asimamisha majadiliano

Spika huyo amesimamisha majadiliano yote katika bunge na kusitisha shughuli za kamati zote na kuamuru wabunge warudi nyumbani, mpaka pale mwanasheria wa serikali atapoweka kando amri ya mahakama ambayo spika ameiita ni upuuzi.

Bunge lilikuwa limevurugika wakati wabunge wakimpuuza mwanasheria mkuu wa serikali aliyekuwa anashikilia amri ya mahakama iheshimiwe.

Spika Kadaga amesisitiza kuwa utaratibu wa bunge lazima ufuatwe na kuwa bunge ni lazima liheshimiwe.

Vurugu katika ukumbi wa bunge

Ukumbi wa bunge ulikuwa umejaa makelele wakati mwanasheria wa serikali alipokuwa ananang’ania kuwa bunge linakaidi amri ya mahakama.

Vincent Isepai, ni wakili wa maswala ya katiba anasema agizo la naibu jaji mkuu ni dharau kwa taifa na kwa sheria.

Wakili Isepai, anashangaa jinsi wakili wa tume ya uchaguzi, ambayo ni idara ya serikali, anavyoweza kufika mahakamani kupinga juhudi zinazofanywa na bunge dhidi ya ufisadi.

Waziri wa maadili ya taifa askofu Simon Lokodo, amelitaja sakata hilo kuwa ni uovu mkubwa katika jamii unaostahili kukemewa na kila mtu, akitaka wahusika wote kufutwa kazi.

XS
SM
MD
LG