Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 01:55

Washitakiwa wa ulipuaji mabomu Uganda wafungwa


Waathirika katika mlipuko wa mabomu uliotokea kwenye mgahawa mmoja katika eneo la Kabalagala mjini Kampala. 11 July 2010
Waathirika katika mlipuko wa mabomu uliotokea kwenye mgahawa mmoja katika eneo la Kabalagala mjini Kampala. 11 July 2010

Jaji mmoja nchini Uganda ametoa hukumu kwa watuhumiwa wawili waliohusika na ulipuaji mabomu mjini Kampala

Jaji mmoja nchini Uganda amewahukumu raia wawili wa nchi hiyo adhabu ya kifungo kwa kuhusika kwao katika ulipuaji wa mabomu ambayo yaliwauwa watu 76 mjini Kampala Julai mwaka jana.

Kundi la waasi la al-Shabab la nchini Somalia lilidai kuhusika kwa mabomu ya kujitoa mhanga ambayo yalilenga kundi la watu ambao walikusanyika kutazama fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010.

Ijumaa, jaji alimhukumu Edris Nsubuga kifungo cha miaka 25 jela kwa mashtaka ya ugaidi. Muhamoud Mugisha alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kupanga njama za ugaidi. Wanaume wote wawili walikiri makosa mwanzoni mwa wiki hii.

Waendesha mashtaka wamesema watawaita watu hao kutoa ushahidi katika kesi zijazo za washukiwa 12 wengine kuhusiana na ulipuaji wa mabomu mjini Kampala.

Al-Shabab ilisema shambulizi lilikuwa la kulipiza kisasi dhidi ya Uganda, kwa jukumu la serikali ya kampala katika jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika linaloisaidia serikali ya Somalia katika mapigano yake dhidi ya waasi wa ki-Islam wenye msimamo mkali wanaojaribu kuchukua madaraka huko Mogadishu.

Ulipuaji mabomu wa Kampala ni shambulizi kubwa la kwanza kufanywa na al-Shabaab nje ya Somalia.

XS
SM
MD
LG