Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 03:22

AU:Uganda yaimarisha ulinzi


Uganda imejiandaa vilivyo kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Afrika unaoanza leo, siku ya Jumatatu katika mji mkuu Kampala.

Uganda imejiandaa vilivyo kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Afrika, ambapo maandalizi yanaanza leo, siku ya Jumatatu katika mji mkuu Kampala. Akizungumza Sauti ya Amerika, waziri wa Kilimo na Uvuvi, Hope Mwesigye amesema serikali ya Museveni iko imara licha ya mashambulizi ya mabomu yaliyotokea wiki iliyopita yaliyouwa zaidi ya watu 70.

Waziri Mwesigye anasema mada kuu ya mkutano huo ni afya ya kina mama na watoto. Lakini anaongeza kuwa mada hiyo ina uhusiano wa karibu na usalama wa chakula na lishe bora.

Marais wengi na viongozi wa serikali wanatazamiwa kushiriki katika mkutano huo, utakaozungumzia pia masuala ya amani, miundombinu, nishati, kilimo na usalama wa chakula.

Baadhi ya wafuatiliaji wameeleza khofu kuwa huenda mkutano huu wa Umoja wa Afrika ukawa lengo la mashambulizi mengine ya wanamgambo hao wa Somalia.
Lakini waziri huyo anawahakikishia wajumbe kuwa Uganda imeweka ulinzi wa hali ya juu wakati wa mkutano huo kwa usalama wao.

Aidha waziri huyo anasema Uganda imepata msaada kutoka kwa washirika wake na wanaamini kuwa mji wa Kampala ni salama.

XS
SM
MD
LG