Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 17:06

Uganda itaahirisha uchaguzi iwapo janga la Corona halitadhibitiwa-Museveni


Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba huenda uchaguzi mkuu nchini humo ukaahirishwa iwapo janga la virusi vya Corona litakuwa halijadhibitiwa.

Katika mahojiano na televisheni ya kibinafsi nchini Uganda NBS, Museveni amesema kwamba "itakuwa hatua ya Mwenda wazimu kuandaa uchaguzi mkuu wakati kuna janga la virusi vya Corona."

Amesema iwapo maambukizi hayo hayatakuwa yamedhibitiwa kufikia mwezi Julai mwaka huu, itabidi mipango ya kuandaa uchaguzi mkuu uliopangwa februari mwaka ujao, itathminiwe upya.

Wagombea 24 wametangaza nia yao ya kuwania urais nchini Uganda.

Kabla ya mlipuko wa virusi vya Corona, wagombea hao walikuwa wameanza mikutano na wafuasi wao mashinani, kujitayarisha kwa uteuzi na tume ya uchaguzi.

Mikutano hiyo imesitishwa.

Miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais ni mwanamziki ambaye pia ni mbunge Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, anayeonekana kama mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni ambaye ametawala Uganda tangu mwaka 1986.

Baadhi ya wagombea wa urais wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka mablimbali mahakamani, akiwemo Bobi wine, aliyefunguliwa mashtaka ya kupanga njama za kuipindua serikali yake Museveni.

Generali Henry Tumukunde, ambaye pia alitangaza mipango ya kuwania urais, ameachiliwa kwa dhamana wiki hii, baada ya kufunguliwa mashtaka ya kupanga kuipindua serikali.

Generali Tumukunde, ambaye alikuwa Rafiki wa karibu sana wa Museveni na hata kuwa waziri wa usalama, ameachiliwa baada ya kuzuiliwa kwa mda wa miezi miwili.

Museveni amesema kwamba watu wanaochanganya siasa na njama za kutaka kupindua utawala wake ndio wanaokamatwa pekee.

-Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG