Suala la ugaidi limeanza kutathminiwa tofauti kutokana na mashambulizi yaliyofuatana katika nchini za Uturuki, Iraq na Saudi Arabia yaliyotokea mwishoni mwa mwezi wa sita na mwanzoni mwa mwezi huu .
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza hali ya usalama duniani kuwa ni tete na kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuongezwa ili kuimarisha usalama katika nchi mbalimbali duniani.
Mchambuzi wa masuala ya usalama kutoka Scotland Evarist Chahali, anasema dunia inapaswa kushirikiana katika masuala ya usalama.
Kufuatia hali ya wasiwasi Marekani imetoa hali ya tahadhari kwa raia wake wanaosafiri nje ya nchi, huku baadhi ya mashirika ya ndege kama vile Emiret yakitahadharisha wasafiri kutotumia mavazi yanayoweza kuleta hisia nyingine.
Makundi kama vile Islamic State, Al qaida na Al shaabab kwa upande wa Afrika yamehatarisha usalama wa watu na mali zao.