Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 21:38

Ufunguo wa nyuklia ni nini?


Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ametuma ujumbe wa Tweet Jumanne kumjibu Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akisema ufunguo wake wa silaha za nyuklia ni mkubwa zaidi kuliko ule wa Kim.

Ukweli ni kuwa hakuna kitu kama ufunguo wa nyuklia.

Kila nchi yenye kujihami na silaha ya nyuklia ina mfumo wake wakupiga silaha hiyo, lakini aghlabu inamtaka kiongozi wa serikali hiyo kujitambulisha kabla ya kuruhusu utumiaji wa silaha hiyo.

Katika nchi ya Marekani hatua ya kupiga silaha ya nyuklia ni siri na ni mchakato mrefu ambao unahusisha utumiaji wa kitu kinachofanana na ‘mpira wa miguu,” ni begi lenye uzito wa pound 45 ambalo linabebwa na mafisa wa jeshi kwa zamu ambao wanafuatana na rais popote anapokwenda.

Begi hilo lina vifaa vya mawasiliano na karatasi yenye maelezo ya matumizi vya vifaa hivyo ikiwemo mpango mzima wa vita. Karatasi hiyo ina majina ya maeneo ambayo yanaweza kulengwa silaha za nyuklia 900 za jeshi la Marekani.

Iwapo Trump ataagiza shambulizi la vita, atajitambulisha kwa maafisa wa jeshi kwa ishara maalum, ambazo zimerikodiwa katika kadi iliyopewa jina la “biscuit” ambayo rais anatembea nayo kila wakati. Rais atatuma ujumbe wa kushambulia kwenye Wizara ya Ulinzi Washington na Kituo cha Mikakati cha kijeshi kilichoko katika jimbo la Nebraska.

Rais hahitaji ruhsa ya mtu yoyote, ikiwemo Bunge la Marekani na Majeshi ya Marekani kutoa idhini ya kufanya shambulio la nyuklia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG