Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 14:29

Ufaransa yatangaza kukamatwa kwa kiongozi wa juu wa Islamic State Mali


Ramani ya Mal
Ramani ya Mal

Ufaransa imetangaza Jumatano wanajeshi katika operesheni za kupambana na wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali katika eneo la Sahel huko Afrika Magharibi imemkamata Oumeya Ould Albakaye, kiongozi wa juu wa kundi la Islamic State nchini  Mali.

Wizara ya Ulinzi ya Vikosi vya Ufaransa imesema Albakaye alikamatwa katika operesheni za Barkhane kati ya usiku wa june 11 na majira ya alfajiri ya juni 12 karibu na mpaka wa Mali na Niger.

Uhusiano mbaya baina ya Ufaransa na jeshi katika koloni lake la zamani la Mali umesababisha Ufaransa kuondoa vikosi vyake vilivyopelekwa huko mwaka 2013 kuwasukuma nyuma wanamgambo wenye uhusiano na al-Qaida na baadae kwa Islamic state.

Mali imegubikwa na ghasia tangu mwaka 2012 wakati jeshi lilipochukua madaraka upande wa kaskazini.

Ufaransa ilikabiliana nao lakini mwaka 2015 walijipanga tena na kuanzisha wimbi la mashambulizi.

XS
SM
MD
LG