Akizungumza baada ya mazungumzo na kiongozi wa kijeshi Kapteni Ibrahim Traore, waziri mdogo Chrysoula Zacharopoulou alisema Ufaransa hailazimishi chochote Burkina Faso, na kwamba hakwenda kushawishi chaguo au uamuzi wowote kutokana na kutokuwepo mtu anayeweza kulazimisha maamuzi ya Burkina Faso.
Aliongeza kusema kwamba Ufaransa itaendelea kujitolea katika kila Nyanja kuanzia za kibinadamu, usalama, na maendeleo, sambamba na upeo na muundo unaotakiwa na serikali ya Burkina Faso.
Alisisitiza kwamba msaada wa Ufaransa unategemea kusikiliza kwa heshima, na unyenyekevu.
Ikiwa ni moja ya nchi maskini zaidi na tete barani Afrika, Burkina Faso inakabiliwa na uasi wa wanajihadi ambao uliibuka kutoka nchi jirani ya Mali, 2015.
Maelfu ya watu wameuawa na karibu milioni mbili wamekimbia makazi yao, na kusababisha mgogoro wa usalama na kibinadamu ambao mwaka jana ulichochea mapinduzi mawili.
Zaidi ya theluthi moja ya nchi iko nje ya udhibiti wa serikali.
Ufaransa, mshirika wa jadi wa nchi zinazozungumza Kifaransa katika Sahel, inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wakosoaji wanaoituhumu kwa ukoloni mamboleo na sasa wanataka uhusiano wa karibu na Moscow.
Katika maandamano ya Septemba 30 ambayo yalimuweka Traore mwenye umri wa miaka 34 madarakani, yakiwa na ghasia yalilenga ubalozi wa Ufaransa mjini Ouagadougou na baadhi ya waandamanaji waliinua bendera ya Russia.
Facebook Forum