Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 12:03

Ufaransa yapokea rasmi barua kutoka Burkina Faso ya kuondoa wanajeshi wake


Ufaransa imepokea rasmi maombi kutoka kwa utawala wa kijeshi wa Burkina Faso ukiitaka  kuondoa wanajeshi wake katika nchi hiyo ya Sahel na imeeleza itafanya hivyo katika kipindi cha mwezi mmoja, wizara ya mambo ya nje imesema Jumatano. 

Msemaji wa wizara amesema Jumanne, wamepokea taarifa rasmi kutoka kwa serikali ya Burkina Faso ikitaka kusitishwa kwa makubaliano ya 2018 juu ya vikosi vya kijeshi vya Ufaransa kuwepo nchini humo.

Amesema kulingana na misingi ya mkataba huo, usitishaji huo unaanza mwezi mmoja baada ya kupokea taarifa ya maandishi, na kwamba wataheshimu misingi ya makubaliano kwa kuzingatia ombi hilo.

Takriban wanajeshi 400 wa kikosi maalumu cha Ufaransa wako Burkina Faso, kinachojulika kama "Sabre," sehemu ya uwepo wa kijeshi ili kupambana na wanajihadi katika eneo lote la Sahel.

Lakini nchi hiyo imefuata mkondo kama ule wa nchi jirani ya Mali, kuingia katika mgogoro na Paris baada ya mapinduzi ya kijeshi na uwepo wa Ufaransa kutofurahiwa na umma.

Serikali ya Burkina Faso imeihakikishia Paris kwamba haitaifuata mkondo wa Mali kwa kugeukia kundi la Wagner la Russia kulisaidia jeshi lake licha ya timu ya mawasiliano kutoka katika kundi hilo la mamluki ikiwa tayari imefanya ziara nchini humo.

Chanzo kinachofahamu mipango ya kijeshi ya Ufaransa kiliiambia AFP kwamba wakati wanajeshi watakapo ondoka mwishoni mwa Februari, vifaa vyao vitachukuliwa mwishoni mwa Aprili.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG