Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 17:57

Ufaransa yaondoka rasmi Burkina Faso


Mkuu wa jeshi la Burkina Faso, Kanali Adam Nere, akipokea bendera kutoka Luteni Kanali wa jeshi la Ufaransa, Louis Lecacheur wakati wa makabidhiano kuashiria kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa, Burkina Faso, katika kambi ya Kamboincin, Burkina Faso, Feb. 18, 2023.

Ufaransa na Burkina Faso zimesimamisha rasmi operesheni za jeshi la Ufaransa katika taifa hilo la Afrika Magharibi, limesema jeshi la Burkina Faso Jumapili, baada ya sherehe ya kushusha  bendera ya vikosi vya Ufaransa.

Hapo Januari, Burkina Faso iliipa Ufaransa mwezi mmoja kuondoa vikosi vyake wakati ikimaliza makubaliano ya kijeshi, yaliyoruhusu vikosi vya Ufaransa kupambana na waasi katika himaya yake, ikielezea kuwa nchi itajilinda yenyewe.

Kuondoka kwao kunafungua ukurasa mpya kwa Burkina Faso kukabiliana na makundi ya kislamu yenye uhusiano na Al Qaida na Islamic State, ambayo yamechukua eneo kubwa la ardhi na kusababisha maelfu ya watu kukosa makazi katika eneo pana la Sahel, kusini kidogo mwa jangwa la Sahara.

Katika taarifa, mkuu wa vikosi vya jeshi la Burkina Faso, amesema jeshi lao limeshiriki chini uongozi wa vikosi maalumu vya Ufaransa, Sabre, katika kushusha bendera na kuadhimisha rasmi kumalizika kwa kikosi kazi cha operesheni katika ardhi ya Burkina Faso.

Wizara inayohusika na mambo ya kijeshi ya Ufaransa haikujibu lolote ilipoulizwa kutoa maoni yake.

Kuondoka kwa takriban wanajeshi 400 wa kikosi maalumu cha Ufaransa, nchini Burkina Faso kunafuatia kudorora kwa uhusiano ambao umejumuisha kwa Ouagadougou kuitaka Ufaransa kumuondoa balozi wake.

Mwaka jana maadamano ya kupinga uwepo wa jeshi la Ufaransa, yaliongezeka maradufu kutokana na mtazamo kwamba Ufaransa haikufanya lolote katika kukabiliana na wanamgambo.

Katika wiki zilizopita, makundi madogo ya waandamanaji wanaopinga uwepo wa Ufaransa, yamekuwa yakikutana kila jioni mjini Ouagadougou kuangalia kama kuna dalili za Ufaransa kuondoka.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG