Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 07:02

Ufaransa yaomba uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanahabari wa nchi hiyo nchini Ukraine


Picha ya mwandishi wa habari wa Ufaransa Frederic Leclerc-Imhoff aliyeuawa nchini Ukraine

Ufaransa Jumatatu imeomba uchunguzi ufanyike baada ya mwandishi wa habari wa Ufaransa kuuawa nchini Ukraine wakati gari alilokuwa akisafiria, ambalo lilikuwa linatumiwa kuwahamisha raia karibu na mji wa Sievierodonesk kushambuliwa kwa makombora.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Catherine Colonna ambaye alikuwa nchini Ukraine Jumatatu, alisema katika taarifa “ Ufaransa inaomba uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo na kwa uwazi kuhusu mazingira ya tukio hilo baya.”

Frederic Leclerc Imhoff, mwenye umri wa miaka 32, ni mwandishi wa habari wa hivi karibuni kuuawa tangu Russia iivamie Ukraine mwezi Februari, alikuwa katika safari yake ya pili kuripoti kwa niaba ya kituo cha televisheni cha Ufaransa BFM nchini Ukraine, kituo hicho kimesema.

Gavana wa mkoa wa Luhansk nchini Ukraine, Serhiy Haidai, amesema katika ujumbe wa maandishi kwenye mtandao wa Telegram kwamba gari la kivita lilishambuliwa na kombora la Russia, na kumua mwandishi wa habari.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Leclerc-Imhoff ni mwanahabari wa 32 kuuawa tangu kuanza kwa uvamizi wa Russia tarehe 24 Februari.

“Natuma rambi rambi zangu kwa wafanyakazi wenzake Frederic na familia yake,”Zelenky amesema katika ujumbe wake wa kila usiku kwa njia ya video.

Wizara ya mambo ya nje ya Russia haikujibu mara moja ombi la Reuters la kutoa maelezo juu ya tukio hilo.

Moscow inakanusha mara kwa mara kwamba wanajeshi wake wanawalenga raia nchini Ukraine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG