Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 07:17

Ufaransa yamkamata kiongozi wa waasi wa Rwanda


Callixte Mbarushimana aliyetiwa mbaroni huko Ufaransa.
Callixte Mbarushimana aliyetiwa mbaroni huko Ufaransa.

ICC inasema Ufaransa imemkamata kiongozi mmoja wa kundi la waasi wa Rwanda anayetuhumiwa kwa ubakaji wa genge huko DRC.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC, inasema maafisa wa Ufaransa wamemkamata kiongozi mwandamizi wa kundi moja la uasi la Rwanda lililoshutumiwa kwa ubakaji uliofanywa na genge la waasi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Taarifa ya ICC inasema Callixte Mbarushimana, kiongozi wa uasi wa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda-FDLR, alikamatwa huko Paris Ufaransa.

ICC inasema Mbarushima anashitakiwa kwa makosa 11 ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo ubakaji, mauaji, manyanyaso ya kijinsia na uharibifu mkubwa wa mali.

FDLR ni moja ya makundi yalioshutumiwa kwa kuwabaka mamia ya watu katika kijiji kimoja mashariki mwa Congo Agosti iliyopita.ICC imesema waasi hao wamefanya uhalifu wa hali ya juu dhidi ya raia huko mashariki mwa Congo kwa miaka kadhaa.

XS
SM
MD
LG