Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 00:42

Ufaransa yakata tiketi ya kuingia nusu fainali ya kombe la dunia


Olivier Giroud wa Ufaransa akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Uingereza. REUTERS.

Timu ya taifa ya Ufaransa -Le Bleu  imekuwa ya pili kukata  tiketi yake ya kucheza nusu fainali ya kombe la dunia baada ya kuifunga Uingereza bao 2-1 katika uwanja wa Al Thumama.

Iliwachukua Ufaransa dakika 17 tu kupata bao lao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji Aurelien Tchouameni

Na Uingereza waliendelea kupambana na katika dakika ya ..ya kipindi chab pili walifanikiwa kupata penati na Harry Kane alisawazisha katika dakika ya 54.

Ufaransa waliendelea na mashabulizi na kujipatia bao la pili katika dakika ya 78 mpira wa kichwa uliopigwa na Olivier Giroud ulikwenda moja kwa moja na kutinga wavuni kutokana na makosa yaliofanywa na Harry Maguire.

Uingereza itabidi wajilaumu wenyewe kwani walikosa penalti ambayo wangeweza kusawazisha baada ya Harry Kane kupiga juu mpira huo na kutoa mpira nje.

Kwa maana hiyo sasa ufaransa itakwaana na wawakilishi pekee wa Afrika Morocco katika nusu fainali ya pili Jumatano Desemba 14.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG