“Hatokuwa tena Mfaransa kwa mtoto wa wazazi wa Kifaransaa,” Darmanin aliwaambia waandishi wa habari alipowasili kisiwani humo, na kutangaza kuondolewa kwa uraia wa kuzaliwa ikiwa ni jambo la kwanza katika historia ya hivi karibuni ya Ufaransa.
Likiwa karibu na visiwa maskini vya Comoro karibu na mwambao wa Afrika Mashariki, koloni hilo la zamani la Ufaransa limekuwa kitovu cha machafuko makali ya kijamii, huku wakazi wengi wakilaumu uhamiaji wasio na vibali kwa hali hiyo kuwa mbaya.
Mayotte, ambayo ni maskini zaidi kuliko Ufaransa, imetikiswa na ghasia za magenge ya uhalifu.
Forum