Kufungwa kwa ubalozi huo mjini Niamey kunaashiria kufungwa kwa moja ya kurasa katika kumaliza uwepo wa Ufaransa katika koloni lake la zamani kufuatia mapinduzi ya Julai ambayo yameiacha nchi hiyo mikononi mwa uongozi wa kijeshi.
“Ubalozi wa Ufaransa kwa sasa umefungwa mpaka itakapotangazwa” Wizara hiyo ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa , na kuongeza mipango ya shughuli muhimu zikiendelea kufanyika kutoka Paris.
Taarifa hiyo imesema kuwa kwa kipindi cha miezi mitano tangu mapinduzi “ubalozi wetu umekuwa ukikabiliwa na vikwazo vinavyofanya ushindwe kufanyakazi” ikiwemo vizuizi katika utendaji.
Wafanyakazi wengi, akiwemo balozi ambaye alifukuzwa nchini humo na uongozi mpya wa kijeshi, wameondoka muda mrefu kidogo.
Jeshi lilimuondoa madarakani kiongozi alichaguliwa Mohamed Bazoum Julai 26, na kufuta makubaliano na Ufaransa, mshirika wake wa jadi wa masuala ya usalama. Bazoum bado yuko katika kizuizi cha nyumbani.
Mbali na Ufaransa kujiondoa, mataifa mengine ya Magharibi yamebaki Niger.
Marekani ilisema Mwezi Desemba kuwa iko tayari kurudisha mahusiano na Niger kwa masharti ya utawala wa kijeshi iunde serikali ya mpito kurejesha utawala wa kiraia.
Afisa wa Marekani alisema mwezi Oktoba kuwa Washington inabakiza maafisa wa jeshi wapatao 1,000 nchini Niger lakini haitajihusisha tena kufanya mafunzo ya kijeshi au kuwyasaidia majeshi ya Niger
Forum