Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Catherine Colonna aliiambia AFP “ Kuna watu 262 ndani ya ndege hiyo aina ya Airbus 330, wakiwemo zaidi ya watoto wachanga 10.”
Colonna alisema ndege hiyo ilitarajiwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Paris Roissy Charles de Gaulle nyakati za usiku.
Yakiwa mapinduzi ya kijeshi ya tatu katika eneo hilo, Rais wa Niger Mohamed Bazoum aliondolewa madarakani na walinzi wake, hali ambayo ilizusha wasiwasi nchini Ufaransa, mtawala wa zamani wa kikoloni wa Niger na mshirika wake wa muda mrefu.
Baada ya umati wa watu wanaoipinga Ufaransa kukusanyika siku ya Jumapili nje ya ubalozi wa Ufaransa na Niger kuishtumu Ufaransa kupanga njama ya kuingilia kati kijeshi, Paris ilisema Jumanne kwamba itawaondoa raia wake na kusaidia kuwaondoa raia wa Ulaya pia.
Forum