Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 16:14

Ufaransa: Vijana sita wafunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kuhusika na kumkata kichwa mwalimu


Jeneza la mwalimu Samuel Paty anayedaiwa aliuawa kwa kukatwa kichwa na wanafunzi likiondolewa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sorbonne wakati wa tukio la kumbukumbu ya kitaifa, Oktoba 21, 2020 in Paris.
Jeneza la mwalimu Samuel Paty anayedaiwa aliuawa kwa kukatwa kichwa na wanafunzi likiondolewa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sorbonne wakati wa tukio la kumbukumbu ya kitaifa, Oktoba 21, 2020 in Paris.

Vijana sita walifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu katika kesi iliyofanyika kwa faragha kwa tuhuma za kuhusika na kumkata kichwa mwalimu wa historia wa Ufaransa, Samuel Paty na mshukiwa wa Kiislamu mwaka 2020 katika shambulio ambalo liligonga kitovu cha maadili ya kidini nchini humo.

Mwalimu alikuwa amewaonyesha wanafunzi wake katuni za Mtume Mohammad katika darasa la uhuru wa kujieleza, jambo lililowakasirisha wazazi kadhaa wa dini ya Kiislamu. Waislamu wanaamini kwamba taswira yoyote ya Mtume ni kufuru.

Mmoja wa watoto hao ni msichana mwenye umri wa miaka 15 ambaye inadaiwa aliwaambia wazazi wake kwamba Paty alikuwa ameonyesha michoro ya mtume huyo katika darasa lake. Atashtakiwa kwa shtaka la uongo baada ya kuthibitishwa kuwa hakuwa darasani wakati huo.

Paty, 47, aliuawa nje ya shule yake katika kitongoji cha Paris na mshambuliaji mwenye umri wa miaka 18, mzaliwa wa Russia mwenye asili ya Chechnya, ambaye alipigwa risasi na polisi mara baada ya shambulio hilo.

Watoto wengine watano watakaofunguliwa mashitaka, walikuwa kati ya miaka 14 na 15 wakati wa shambulio hilo, watashtakiwa kwa kula njama ya uhalifu uliokusudiwa.

Wanashukiwa kuelekeza wauaji kwa Paty au kusaidia kufuatilia jinsi anavyotoka shuleni.

Watoto wote sita walipelekwa katika mahakama ya watoto na wanaweza kufungwa jela miaka 2.5. Kesi hiyo inayotarajiwa kukamilika Desemba 8, zinafanyika kwa faragha.

Forum

XS
SM
MD
LG