Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 21:19

Ufaransa kufanya uchaguzi jumapili


Rais wa ufaransa Nicolas Sarkozy kabla ya kampeni za uchaguzi

Mdahalo huo uliofanyika siku moja baada ya kiongozi wa mrengo wa kulia Marine Le Pen aliyeshika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwezi uliopita kusema kuwa hatamuunga mkono mgombea yoyote katika uchaguzi wa marudio.

Rais wa ufaransa Nicolus Sarkozy na mpinzani wa kisoshalist Francois Hollande wamechuana katika mdahalo pekee kabla ya duru ya pili ya uchaguzi jumapili hii ambapo bwana hollande anatarajiwa kushinda.
Katika mdahalo wa jumatano ulionyeshwa kwenye televisheni bwana Sarkozy na bwana Hollande walishutumiana kila mmoja kwa kudanganya wakati wakizungumzia kuhusu sera zao za uchumi.
Katika kampeni bwana Hollande alimshutumu bwana Sarkozy kwa kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira nchini ufaransa ambacho ni karibu asilimia 10 na kutoa mwito wa mabadiliko makubwa katika kuboresha masuala ya fedha nchini humo.
Mdahalo huo uliofanyika siku moja baada ya kiongozi wa mrengo wa kulia Marine Le Pen aliyeshika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwezi uliopita kusema kuwa hatamuunga mkono mgombea yoyote katika uchaguzi wa marudio.
Bwana Hollande aliibuka mshindi katika upigaji kura wa kwanza dhidi ya bwana Sarkozy ambaye ameongoza nchi kwa miaka mitano na kushutumiwa kwa kuchukua hatua kali za kiuchumi ili kupunguza deni la ufaransa.
Bwana Hollande ni mwanasiasa mkongwe anayeongoza chama cha socialist kwa miaka mingi lakini hajawahi kushika nafasi ya juu ya uongozi serikalini.

XS
SM
MD
LG