Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 11:53

Aleksander Ceferin ndiye Rais mpya wa UEFA


Aleksander Ceferin aliechaguliwa kuwa Rais mpya wa UEFA kutoka Slovenia.

Shirikisho la soka la Ulaya UEFA, Jumatano limemteuwa Aleksander Ceferin kutoka Slovenia kuwa Rais wake mpya.

Shirikisho la soka la Ulaya UEFA, Jumatano limemteuwa Aleksander Ceferin kutoka Slovenia kuwa Rais wake kwa wingi mkubwa wa kura 42 dhidi ya 13. Ceferin sasa atachukua wadhifa huo kutoka kwa Michael Platini kutoka Ufaransa, aliyeondolewa bila kukamilisha muda wake baada ya kupigwa marufuku kwa miaka minne kushiriki katika uongozi wa kandanda mwezi Mei kutokana na madai ya kukiuka maadili.

Ceferin alimshinda makamu Rais wa UEFA Michael van Praag aliye kuwa mpinzani pekee na ambae sasa atakuwa madarakani ili kumaliza kipindi cha Platini kitakachomalizika 2019. Kabla ya kuchaguliwa kama kiongozi wa UEFA, Ceferin mwenye umri wa miaka 48 alikuwa kiongozi wa shirika la soka la Slovenia na hajawahi kuwa kwenye kamati ya UEFA.

Licha ya kupigwa marufuku , Platini aliruhusiwa kuwahutubia wajumbe wa UEFA wakati wa hafla hiyo Jumatano akiwashukuru wote kwa kushirikiana nae na kusisistiza kwamba hakufanya kosa lolote na ataendelea kupambana kisheria.

XS
SM
MD
LG