Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 10, 2024 Local time: 18:48

Uchunguzi wanaendelea na uchunguzi wa jaribio la mauaji ya Trump


Wachunguzi wa Marekani wanapekuwa akaunti za mitandao ya kijamii na matangazo mengine ya mshukiwa wa jaribio la Jumapili la mauaji ya Rais wa zamani Donald Trump, wakijaribu kubaini nia na iwapo kuna mtu mwingine yeyote anaweza kuwa amehusika.

Polisi wa Florida walimkamata Ryan Wesley Routh mwenye umri wa miaka 58, baada ya kumsimamisha barabarani Jumapili takriban saa moja au zaidi baada ya kutoroka kwenye Klabu ya Gofu ya Rais wa zamani ya Trump, mjini West Palm Beach, Florida.

Maafisa wamesema taarifa zilizokusanywa kwenye simu ya Routh zilionyesha alikaa na kusubiri kwa saa 12, akijificha kwenye vichaka kando ya uzio.

Routh ameshtakiwa na serekali kuu kwa kukutwa na bunduki akiwa ni mhalifu na kumiliki bunduki yenye nambari maalumu iliyofutwa.

Forum

XS
SM
MD
LG