Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 05:34

Uchunguzi wafanyika Burkina Faso wa madai ya njama za kuvunja amani


Mamlaka zilikuwa zinachunguza jaribio jipya la kuvuruga amani nchini  Burkina Faso, ambalo limemhusisha afisa mwandamizi  mwenye uzoefu na sifa kubwa, kulingana na mwendesha mashtaka wa kijeshi. 

Mamlaka zilikuwa zinachunguza jaribio jipya la kuvuruga amani nchini Burkina Faso, ambalo limemhusisha afisa mwandamizi mwenye uzoefu na sifa kubwa, kulingana na mwendesha mashtaka wa kijeshi.

Moja ya nchi maskini sana duniani, Burkina Faso tayari imeshuhudia mapinduzi mawili yaliyofanywa na maafisa wa jeshi waliochukizwa mwaka huu ambayo yameliweka jeshi madarakani.

Mwendesha mashitaka alisema katika taarifa yake kwamba hatua za kwanza za uchunguzi zilianzishwa baada ya habari kutoka kwa mtoa taarifa aliyebaini kwamba wanajeshi walikuwa wakijiandaa kuvuruga taasisi za serikali.

Miongoni mwa waliopanga njama hizo ni afisa mkuu wa hati za ukamataji Charles Neboa na sajenti Adama Traore, kulingana na mtoa taarifa aliyenukuliwa katika taarifa hiyo.

Mwendesha mashitaka Kapteni Ibrahim Traore alisema, maafisa hao waliwasiliana na kitengo cha 'Green Mamba' cha luteni-Kanali Emmanuel Zoungrana, na walikusudia kuanzisha mashambulizi ya sambamba kwenye redio na televisheni ya Burkina Faso (RTB), gereza la kijeshi Maca, ambako afisa huyo alikuwa anashikiliwa kwa vitendo kama hivyo, na makazi ya mkuu wa nchi.

Zoungrana alikamatwa Januari 14 akishukiwa kwa jaribio la kuvuruga taasisi za serikali na orodha ndefu ya mashtaka ikiwa ni pamoja na wizi, kughushi na utakatishaji fedha.

XS
SM
MD
LG