Wachunguzi wanatarajiwa kuwasili Syria hivi karibuni.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayofanya uchunguzi huo imesema kwamba maafisa wa Syria wanashirikiana vyema katika uchunguzi huo baada ya kukubali uchunguzi ufanyike katika ziara ya wachunguzi ya hivi karibuni mjini Damascus.
Tume ya uchunguzi inaongozwa na Robert Petit.
Wachunguzi watasaidia katika kukusanya ushahidi na kuwafungulia mashtaka wahusika kuhusiana na uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki ya watu nchini Syria tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011
Raia wa Syria wamekuwa wakitaka uchunguzi kufanyika na wahusika wa uhalifu dhidi ya ubinadamu kufunguliwa mashtaka, tangu waasi walipopindua serikali ya rais Bashar al-Assad.
Forum