Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 04, 2023 Local time: 23:05

Uchunguzi wa maoni unabashiri ushindi kwa Museveni


Rais Museveni mwenye kofia akimpa mkono hasimu wake wa kisiasa Besigye.

Uchunguzi wa mwisho wa maoni uliotolewa na tasisi ya Research World International unaonesha kwamba Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wa chama tawala cha National Resistance Movement-NRM anaweza kushinda kwenye uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika Februari 18 mwaka huu kwa asilimia 51 za kura.

Dr.Kiiza Besigye wa chama kikuu cha upinzani cha Forum for Democratic Change-FDC anatarajiwa kushika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 32 huku mgombea huru na Waziri Mkuu wa zamani, Patrick Amama Mbabazi anatarajiwa kushika nafasi ya tatu kwa asilimia 12.

Patrick Amama Mbabazi
Patrick Amama Mbabazi

Uchunguzi huo wa maoni ulifanya kati ya Januari 15 hadi 19 ambapo uliwashirikisha wapigakura 2,685 katika wilaya 89 kote Uganda.

Mkurugenzi mkuu wa Research World International, Patrick Wakida alisema uchunguzi huo ulifanyika kwa njia ya kisayansi kabisa na kumulika hali ilivyo katika kinyang’anyiro cha kiti cha urais, bunge na serikali za mitaa.

XS
SM
MD
LG