Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:36

Uchunguzi wa ajali ya ndege ya MH 17 wakaribia kutolewa


Waendesha masitaka wa Uholanzi wanasema uchunguzi wa ushirikiano wa kimtaifa wa kuangushwa kwa ndege ya MH17 kwenye anga ya mashariki mwa Ukraine umefikia katika hatua ya juu sana na matokeo yatatolewa katika miezi michache ijayo.

Sehemu hii ya uchunguzi ni juu ya silaha iliyotumika na eneo hasa iliporushwa kuweza kuangusha ndege ya Malaysia.

Ndege hiyo ilianguka katika eneo la waliojitenga wanaoungwa mkono na Russia Julai 17, 2014 na kuuwa watu wote 298 waliokuwa kwenye ndege hiyo ambao theluthi mbili walikuwa raia wa Uholanzi.

XS
SM
MD
LG