Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 09:14

ICC kuchunguza ripoti za ghasia Burundi


Polisi na wanajeshi nchini Burundi wakiwafurusha waandamanaji.
Polisi na wanajeshi nchini Burundi wakiwafurusha waandamanaji.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) itachunguza ripoti za mauaji, mateso, ubakaji na uhalifu mwingine uliotendeka wakati wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi mwaka mmoja uliopita.

Vitendo hivyo vinaonekana vipo ndani ya mamlaka ya ICC, mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda alisema katika taarifa yake leo Jumatatu. "Nimeamua kufungua uchunguzi wa awali kuhusiana na hali nchini Burundi. Uchunguzi wa awali si uchunguzi rasmi, bali ni utaratibu wa kuangalia iwapo uchunguzi rasmi ni muhimu. Hakukuwa na majibu ya haraka kutoka serikali ya Burundi."

Taarifa ya Bensouda ilisema kwamba ICC itawasiliana na serikali kwa mtazamo wa kulijadili suala hili. Burundi iliingia katika maandamano na ghasia mwezi Aprili mwaka jana baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutafuta njia ambayo wengi wanaiona kama ukiukaji wa katiba kutaka kuwepo madarakani kwa muhula wa tatu. Tangu wakati huo, zaidi ya watu 400 wameuwawa na 250,000 wamekimbia nchi.

XS
SM
MD
LG