Kutokana na kusimamishiwa kwa misaada kutoka nje ya mabilioni ya dola, serikali inayoongozwa na wanajeshi ilipandisha bei na kodi kwenye kila kitu kuanzia huduma za afya hadi mafuta ya kupikia, ongezeko la bei ambalo limewakera sana wanainchi,
Mzozo wa kiuchumi wa Sudan wa muda mrefu, uliosababishwa na miongo kadhaa ya vita, kutengwa na vikwazo vya kiuchumi, ulionyesha dalili za afueni kabla ya mapinduzi, sasa leo umekuwa tishio kubwa la mzozo mpya wa kibinadamu, wakati wanainchi wake wanakabiliwa na machafuko mengine na ongezeko la viwango vya njaa.
Viongozi wa kijeshi wameshindwa kumteua waziri mkuu na maandamano yamepamba moto kwa miezi kadhaa.
Amin Shibeika ambaye ni mmiliki wa benki mjini Kharthoum anasema, mzozo wa kisiasa unaathiri biashara