Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 07:01

Uchumi wa dunia unajikokota, IMF kusema


Mtu akitembea nje ya makao makuu ya IMF, Washington DC.
Mtu akitembea nje ya makao makuu ya IMF, Washington DC.

Shirika la kimataifa la fedha IMF, limesema Jumanne kwamba uchumi wa dunia uko katika kasi ya pole pole, na wala hakuna dalili za hali hiyo kubadilika kwa haraka.

IMF limesema kwamba inatarajia viwango vya ukuaji kushuka kutoka asilimia 6.1 ilivyokuwa mwaka jana, hadi asilimia 3,2 mwaka huu, ikiwa idadi ya chini kuliko ilivyotabiriwa mwezi Aprili.

Ukuaji uliotarajiwa mwaka jana ulifuatiwa na hali ngumu mwaka huu pale masuala mengi yalipoanza kujitokeza. Uzalishaji wa bidhaa kote ulimwenguni ulishuka kwenye robo ya kwanza ya mwaka huu kutokana na hali huko China na Russia ,wakati pia matumizi ya wanunuzi Marekani yalishuka kuliko ilivyotarajiwa.

IMF yenye makao yake Washington imesema kwamba uchumi wa dunia umepitia misukosuko kadhaa wakati ambapo ulikuwa tayari umepigwa vibaya na athari za janga la corona. Kuna hali ya kushuka kwa thamani ya fedha kote ulimwenguni na hasa hapa Marekani na kwenye mataifa ya Ulaya, hali iliyopelekea masharti magumu ya kiuchumi.

Uchumi wa China pia ulipungua kasi kuliko ilivyotarajiwa kutokana na janga la corona, lililopelekea kufungwa kwa shughuli za kawaida na hatimaye uvamizi wa Russia nchini Ukraine. IMF imesema kwamba bei za bidhaa muhimu kama chakula na mafuta zimeendelea kupanda kote ulimwenguni. Gharama ya maisha inakisiwa kupanda kwa asilimia 6.6 kwenye mataifa yaliyoendelea wakati asilimia 9.5 ikitarajiwa kwenye mataifa yanayoendelea.

XS
SM
MD
LG