Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 21:53

Uchumi wa China kupanda tena baada ya Corona


Sehemu ya mji wa Sanghai ambapo maisha ya kawaida yameanza kurejea
Sehemu ya mji wa Sanghai ambapo maisha ya kawaida yameanza kurejea

Serikali ya China imesema kwamba uchumi wa taifa ulishuka kwenye kipindi cha miezi mitatu kufikia Juni, kutokana na kufungwa kwa shughuli za kawaida kutokana na corona.

Taarifa zinasema kwamba mji wa Shanghai pamoja na miji mingine ilifungwa kufuatia mlipuko mpya wa virusi vya corona, ikiongeza kusema kwamba kuna matumaini ya kujikwamua sasa kwa kuwa hali ya kawaida imerejea.

Hatua za kuzuia maambukizi zilipelekea kufungwa kwa Shanghai ambapo kuna bandari yenye shughuli nyingi zaidi kwenye taifa hilo la pili kwa uchumi duniani, na kuzua wasi wasi wa kuathirika kwa biashara za kimataifa pamoja na viwanda.

Mamilioni ya familia pia zililazimika kubaki nyumbani na kwa hivyo kuathiri soko la bidhaa nchini humo. Chama tawala cha kikomunisti kimeahidi misamaha ya kodi, kutolipa kodi za nyumba kwa muda, pamoja na misaada mingine ya kifedha ili kusaidia biashara kurudi kwenye hali ya kawaida.

Baadhi ya wafanyabashara wadogo kama wa migahawa na maduka wamefunga biashara zao, huku waliobaki wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi kutokana na janga hilo.

XS
SM
MD
LG