Waziri mkuu wa visiwa hivyo Manasseh Sogavare, amesema kwamba kucheleweshwa huko kwa uchaguzi kwa muda wa miezi 7, kunahitaji marekebisho ya kikatiba, na ni kwa sababau taifa hilo ni mwenyeji wa michezo ya kimataifa ya Pacific, mwaka ujao.
Amasema kwamba kufanya uchaguzi sambamba na michezo hiyo kutagharimu hela nyingi pamoja na kuzua changamoto za kiufundi. Hata hivyo kiongozi wa upinzani Mathew Wale amesema kwamba hatua hiyo inahujumu haki ya wananchi ya kupiga kura mwaka ujao.
Ameongeza kusema kwamba ni mbinu ya waziri mkuu ya kubaki madarakani zaidi ya muhula wake. Sagavare amesema kwamba waziri mkuu amesababisha aibu ya kieneo , kama taifa ambalo lipo tayari kukiuka katiba yake ili kuwa mwenyeji wa michezo ya wiki mbili kinyume na matakwa ya wananchi wake.