Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:46

Uchaguzi wa Senegal wakamilika


Rais wa Senegal Abdoulaye Wade akiwa amezungukwa na waunga mkono wake na walinzi akisafiri katika vituo mbali mbali wakati wa kampeni huko Senegal.
Rais wa Senegal Abdoulaye Wade akiwa amezungukwa na waunga mkono wake na walinzi akisafiri katika vituo mbali mbali wakati wa kampeni huko Senegal.

Rais Abdoulaye Wade awakasirisha wasenegal wengi na hatimaye azomewa wakati akipiga kura Jumapili wakati akigombea muhula wa tatu.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa katika uchaguzi wa rais wa Senegal baada ya wiki kadhaa za maandamano ya ghasia yaliosababishwa na kiongozi aliyepo madarakani kutaka kugombea urais kwa muhula wa tatu. Mapema jumapili mamia ya watu walimzomea rais Abdoulaye Wade wakati alipopiga kura katika kituo kilichoko karibu na nyumbani kwake. Bw.Wade amewakasirisha raia wengi wa Senegal kwa kujaribu kuongeza muda wa utawala wake wa miaka 12 kwa muhula mwingine. Wapinzani wanasema uamuzi wake ni kinyume cha katiba kufuatia mabadiliko aliyosaini kuwa sheria mwaka 2001, ambapo rais anatakiwa kuhudumu kwa mihula miwili pekee.

XS
SM
MD
LG